Rasta ni aina za nywele zilizotengenezwa kwa kutumia katani au
wengine wanasema (nywele za wazungu). Nywele hizo huuzwa katika maduka
mbalimbali ya vipodozi na urembo. Hapa Tanzania ndiyo penyewe kwani maduka ya
Rasta yameshona kama utitiri ukianzia Kariakoo hadi katika mitaa.
Kuna aina nyingi za rasta kama Sangita, Angel, Darling na nyinginezo.
Katika aina hizo za rasta Sangita iko juu kwani inauzwa takribani shilingi elfu
3000. Rasta za kawaida ni kuanzia shilingi elfu moja na kuendelea.
Siku hizi wanawake wengi huboresha muonekano wao kwa
kusuka nywele za rasta. Ni hakika huwa wanapendendeza. Wenyewe wanasema
‘mwanamke urembo’.
Zipo staiil mbalimbali za kusuka rasta kama vile vitunguu,
yeboyebo, njia tatu, mkeka na nyinginezo. Wanawake wengi wanapendelea yeboyebo
na njia tatu kwa sababu ndiyo huvutia zaidi.
No comments:
Post a Comment